Skip to main content

MAMBO KUMI MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UJENZI WA NYUMBA YAKO


Ujenzi wa nyumba si lele mama. Watu wengi wanaanza ujenzi na wanashindwa kumaliza au hata wakimaliza,  wanamaliza kwa taabu sana. Nikiwa kama mdau wa ujenzi na mtu ambaye nimepitia changamoto hii ya ujenzi na kwa uzoefu mbali mbali kutoka kwa ndugu na jamaa nimekuandalia kwa ufupi mambo muhimu kumi ambayo ukiyafuata, utaanza na kumaliza ujenzi wako pasi na shida yoyote.
mambo hayo ni kama yafuatayo;

1. Tafuta kiwanja cha gharama nafuu

2. Jenga nyumba yenye ukubwa wa wastani.

3. Tumia nafasi ya eneo la nyumba yako kwa uangalifu.

4. Ni vyema kujenga nyumba yenye ramani ya umbo la mraba au mstatiri.         

5. Anza ujenzi wako kwa kufanya mpangilio mzuri wa mradi wako wa ujenzi, maana                wanasema kufeli kupanga ni kupanga kufeli.

6.Tengeneza ramani yenye muonekano mzuri na rahisi kujenga, epuka ramani tata na           ngumu.

7. Hakikisha unampata fundi mzuri na mzoefu kwa aina ya nyumba unayotaka kujenga.

8.Ni vyema kutumia vifaa na "material" ya ujenzi  yaliyo karibu na eneo lako la ujenzi.

9.Fuatilia kwa ukaribu gharama za ujenzi katika kila hatua ya ujenzi.

10.Kumbuka si wakati wote uchague vitu vya bei rahisi, zingatia ubora kwanza.

Comments